Wapigakura wachache wateremka vituoni Cote dÍvoire
Uchaguzi wa bunge umefanyika Cote dÍvoire hapo jana, lakini idadi ndogo tu ya wapiga kura walijitokeza vituoni. Kiasi ya watu milioni 5.7 waliandikishwa kupiga kura katika uchaguzi huo wa bunge wa kwanza kufanyika nchini humo, tangu mwaka 2000.
Chama cha rais wa sasa Alassane Ouattara, kinatazamiwa kushinda kwa wingi mkubwa, kwani chama cha rais wa zamani Laurent Gbagbo kimeususia uchaguzi huo. Ni mwaka mmoja tu tangu kumalizika kwa uchaguzi wa rais nchini humo.
Uchaguzi huo, ulisababisha machafuko na umwagaji mkubwa wa damu miongoni mwa wafuasi wa Ouattara na wa Gbagbo. Matokeo ya uchaguzi wa jana yanatazamiwa kutangazwa baadae wiki hii. Gbagbo sasa amepelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague, Uholanzi, akikabiliwa na mashtaka ya kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa machafuko kufuatia uchaguzi wa rais.
No comments:
Post a Comment