Monday, 12 December 2011

MGOMO HUKO SYRIA

Wito wa kugoma umeitikiwa Syria

Wito wa upinzani kufanya mgomo mkubwa nchini Syria umeitikiwa katika miji mingi. Wanaharakati wamesema, maduka yalifungwa katika wilaya za Daraa na Idleb na hata katika miji ya Homs na Harasta. Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu wa Syria kutoka London wamesema, vikosi vya usalama nchini Syria vimetumia nguvu kuwalazimisha watu kuyafungua maduka yao. 
Mgomo huo umeitishwa kupinga ukandamizaji unaoendelea kufanywa na serikali ya Syria. Wapinzani hao wametoa mwito pia kuususia uchaguzi wa serikali za mitaa leo hii. Wanaharakati wanasema, tangu jumamosi raia 14 wameuawa na vikosi vya usalama nchini humo.

No comments:

Post a Comment