Makubaliano yapatikana kwenye mkutano wa Durban
Katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, mjini Durban, Afrika Kusini, wajumbe wa mataifa 194 wameukubali mpango uliopendekezwa na Umoja wa Ulaya kurefusha muda wa Mkataba wa Kyoto na kujadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa na wote ili kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua hewa.
Kuambatana na makubaliano hayo, ifikapo mwaka 2015 kupatikane mkataba utakaopaswa kuheshimiwa kisheria na nchi zote na mkataba huo uanze kufanya kazi mwaka 2020.
Kwa maoni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon na hata serikali ya Ujerumani, hayo ni makubaliano ya kihistoria katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini mashirika yanayotetea mazingira kama vile Greenpeace na hata wanasayansi wanasema, makubaliano hayo hayatoshi. Wanaaminui kuwa haitowezekana kuyatimiza malengo yanayoazimia kuzuia ongezeko la joto duniani kupanda kwa zaidi ya nyuzi joto 2 za Celsius.
No comments:
Post a Comment