Monday 12 December 2011

UCHAGUZI WA DRC UNAMASHAKA

Ujumbe wa kimataifa wa wasimamizi wa uchaguzi umeamua kuwa uchaguzi uliofanywa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, si wa kutegemewa.
Tume ya Uchaguzi ya DRC
Rais Kabila alishinda katika uchaguzi huo.
Kituo cha Carter piya kimesema kuwa uchaguzi huo umetiwa dosari, kwa kutotayarishwa sawasawa, na pengine ulikuwa na udanganyifu; na kwamba matokeo ya vituo vya kupigia kura karibu 2000 mjini Kinshasa, yaani asili-mia-20 ya vituo vya mji mkuu, yalipotea.
Wajumbe wake wanasema takwimu rasmi za matokeo ya jimbo la Katanga, kusini mwa nchi, yanaonesha ulalamishi - maeneo mawili yalionesha kuwa Bwana Kabila alipata karibu kura zote.
Kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi, ameyakataa matokeo rasmi yaliyotangazwa, na amejitangaza kuwa yeye ndiye rais.

No comments:

Post a Comment