Siku ya jana majira ya asubuhi baada ya mvua kubwa iliyonyesha maeneo mengi ya jiji hili likiwemo eneo moja lijulikanalo kama shule ya msingi mzambarauni lililopo wilaya ya ilala kata ya ukonga, limetokea tukio moja la kusikitisha na kuuzunisha kwani kipindi mvua hiyo inaendelea kulikuwepo na watu watano waliokuwa chini ya mti wa mwembe wakijisitiri mvua isiweze kuwalowanisha pia miongoni mwao wakisubiri usafiri, ndipo baada ya muda mfupi ulitokea upeepo mkali uliopelekea kuangusha mwembe huo ambao ukaangukia mbuyu hivyo kupelekea kuanguka kwa mwembe pamoja na mbuyu. wote walifanikiwa kuuona pindi unaanza kukatika ndipo watu wanne wakafanikiwa kuukimbia na kukwepa kabla haujaanguka lakini dada mmoja alishindwa hivyo kupeelekea mwembe huo kumwangukia na kupoteza maisha papo hapo, baada ya dakika chache wasamalia wema walifanikiwa kuutoa mwili wa marehemu na kuukimbiza hospital. uchunguzi wa awali ulionyesha marehemu ni mkazi wa eneo hilo la mzambarauni MWENYEZI MUNGU aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi amen. hadi siku ya leo mkakati unaendelea wa kuukata na kuuondoa kabisa mwembe na mbuyu eneo hilo la tukio.
Tuesday, 13 December 2011
Monday, 12 December 2011
MGOMO HUKO SYRIA
Wito wa kugoma umeitikiwa Syria
Wito wa upinzani kufanya mgomo mkubwa nchini Syria umeitikiwa katika miji mingi. Wanaharakati wamesema, maduka yalifungwa katika wilaya za Daraa na Idleb na hata katika miji ya Homs na Harasta. Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu wa Syria kutoka London wamesema, vikosi vya usalama nchini Syria vimetumia nguvu kuwalazimisha watu kuyafungua maduka yao.
Mgomo huo umeitishwa kupinga ukandamizaji unaoendelea kufanywa na serikali ya Syria. Wapinzani hao wametoa mwito pia kuususia uchaguzi wa serikali za mitaa leo hii. Wanaharakati wanasema, tangu jumamosi raia 14 wameuawa na vikosi vya usalama nchini humo.
UCHAGUZI WABUNGE WAJITOKEZA WATU WACHACHE
Wapigakura wachache wateremka vituoni Cote dÍvoire
Uchaguzi wa bunge umefanyika Cote dÍvoire hapo jana, lakini idadi ndogo tu ya wapiga kura walijitokeza vituoni. Kiasi ya watu milioni 5.7 waliandikishwa kupiga kura katika uchaguzi huo wa bunge wa kwanza kufanyika nchini humo, tangu mwaka 2000.
Chama cha rais wa sasa Alassane Ouattara, kinatazamiwa kushinda kwa wingi mkubwa, kwani chama cha rais wa zamani Laurent Gbagbo kimeususia uchaguzi huo. Ni mwaka mmoja tu tangu kumalizika kwa uchaguzi wa rais nchini humo.
Uchaguzi huo, ulisababisha machafuko na umwagaji mkubwa wa damu miongoni mwa wafuasi wa Ouattara na wa Gbagbo. Matokeo ya uchaguzi wa jana yanatazamiwa kutangazwa baadae wiki hii. Gbagbo sasa amepelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague, Uholanzi, akikabiliwa na mashtaka ya kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa machafuko kufuatia uchaguzi wa rais.
MZOZO WAANZA HUKO BURBAN
Makubaliano yapatikana kwenye mkutano wa Durban
Katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, mjini Durban, Afrika Kusini, wajumbe wa mataifa 194 wameukubali mpango uliopendekezwa na Umoja wa Ulaya kurefusha muda wa Mkataba wa Kyoto na kujadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa na wote ili kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua hewa.
Kuambatana na makubaliano hayo, ifikapo mwaka 2015 kupatikane mkataba utakaopaswa kuheshimiwa kisheria na nchi zote na mkataba huo uanze kufanya kazi mwaka 2020.
Kwa maoni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon na hata serikali ya Ujerumani, hayo ni makubaliano ya kihistoria katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini mashirika yanayotetea mazingira kama vile Greenpeace na hata wanasayansi wanasema, makubaliano hayo hayatoshi. Wanaaminui kuwa haitowezekana kuyatimiza malengo yanayoazimia kuzuia ongezeko la joto duniani kupanda kwa zaidi ya nyuzi joto 2 za Celsius.
TUME YA UCHAGUZI KENYA YASIKILIZA HOJA ZA WA KENYA WAISHIO MAREKANI
"Kuna suala la uwandikishaji wapiga kura, jee ni hati gani wanabidi kuonesha kuthibitisha uraia wao?" amesema Omondi
Kenya inapoadhimisha miaka 48 ya uhuru iliyonyakua kutoka Uingereza Disemba 12 1963, Wakenya wanatafakari na kujadili namna ya kutekeleza katiba mpya inayoleta mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii, na haki za kiraia.
Mojawapo ya mabadiliko makubwa ni kuwaruhusu Wakenya wanaoishi katika nchi za nje kuweza kupiga kura katika uchaguzi unaofanyika nchini humo. Na mtihani mkubwa ni uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2012.
Kutokana na hali hiyo, maafisa wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC wakiongozwa na mwenyekiti wa tume Ahmed Issack Hassan, unatembelea miji mikubwa ya Marekani na kusikiliza maoni ya wananchi wa nchi hiyo, ili kutafakari namna ya kupanga zowezi hilo nje ya nchi kwa mara ya kwanza.
UCHAGUZI WA DRC UNAMASHAKA
Ujumbe wa kimataifa wa wasimamizi wa uchaguzi umeamua kuwa uchaguzi uliofanywa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, si wa kutegemewa.
Rais Kabila alishinda katika uchaguzi huo.
Kituo cha Carter piya kimesema kuwa uchaguzi huo umetiwa dosari, kwa kutotayarishwa sawasawa, na pengine ulikuwa na udanganyifu; na kwamba matokeo ya vituo vya kupigia kura karibu 2000 mjini Kinshasa, yaani asili-mia-20 ya vituo vya mji mkuu, yalipotea.
Wajumbe wake wanasema takwimu rasmi za matokeo ya jimbo la Katanga, kusini mwa nchi, yanaonesha ulalamishi - maeneo mawili yalionesha kuwa Bwana Kabila alipata karibu kura zote.
Kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi, ameyakataa matokeo rasmi yaliyotangazwa, na amejitangaza kuwa yeye ndiye rais.
tanzania ikiwainaendelea kusherekea miaka yake 50 ya uhuru wengine waendelea kulia machozi
wakati tanzania ikiendelea kujivunia maadhimisho yake ya miaka 50 ya uhuru kwa upande mwingine wananchi wameendelea ku bubujika machozi makundi hayo ni pamoja na ma albino ambao wamekiri kuwa miaka hiyo kwao ni kama kusherekea kunyanyaswa na kutengwa kwaajili ya ulemavu wao, kundi lingine ni maskini ambao wanachukua nafasi kubwa sana katika nchi hii, kwani imeonekana dhahili kuwa maskini ataendelea kuitwa maskini hadi kifo chake na tajiri kuwa tajiri zaidi. tovuti yetu ilifanya mkakati wa kumtafuta kiongozi yeyote mwenye wadhifa katika serikali yetu kwaajili ya kufahamu kero hii itakwisha lini ya kuweka usawa na kupunguza gepu la tabaka lililopo kati ya maskini na tajiri lakini viongozi walio wengi hawakuweza kuwa na muda wa kulijibu swali hilo. ukweli ni kwamba iko haja ya serikali yetu kuangalia swala hilo na kuwapunguzia makali ya maisha wananchi hasa wale wa kipato cha chini
Subscribe to:
Posts (Atom)