Akizungumza baada ya Algeria kutangaza kuwa mkewe Gaddafi, Safiya pamoja na watoto wawili wa kiume, binti yake na watoto wao wamevuka mpaka na kuingia nchni humo, Msemaji wa waasi, Mahmud Shammam alisema kwamba wangenda watu wote hao warejeshwe.
Mpaka sasa, Algeria haijalitambua baraza la waasi na imekuwa na msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mgogoro wa Libya, hata hivyo miongoni mwa waasi wamekuwa wakihituhumu nchi hiyo kuunga mkono utawala wa Gaddafi.
Katika taarifa iliyotangazwa na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, imetaja majina ya watoto wa Gaddafi ambao wamevuka mpaka Libya na kuingia Algeria kuwa ni Aisha, Hanibar na Mohammed.
Gaddafi akiwa na familia yakeHata hivyo haikutoa ufafanuzi zaidi kuhusu alipo Gaddafi mwenyewe. Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kwamba viongozi mbalimbali tayari wamekwisha fahamishwa kuhusu jambo hilo.
Miongoni wa waliotajwakupata taarifa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Baraza la Usalama la Umoja huo pamoja na Kiongozi namba mbili wa waasi wa Mahmud Jibril.
Akijibu taarifa hiyo, mbele ya waandishi wa habari mjini Tripoli Shammam amesema wanakipokea vyema kitendo hicho na kwamba wanawahakikishia majirani zao hao wanataka uhusiano mzuri baina yao kwa kuhakikisha wanawarejesha."Hicho ni kitendo cha uchokozi dhidi ya watu wa Libya na matumaini yao. Tutachukua njia zote za kisheria ili wahalifu hao warudishwa na baadae tutawapeleka mahakamani" alisema Shammam.
Nalo Shirika la Habari la ANSA, likinukuu vyanzo vya kuaminika vya kidiplomasia vya Libya vikisema Gaddafi Gaddafi na wanawe Saadi pamoja na Seif al-Islam wamejificha katika mji unaoitwa Bani Walid, uliyopo kusini mwa Tripoli.
Katika hatua nyingine Waziri wa Sheria katika Baraza la Waasi, Mohammed al-Allagy amesema mtoto wa mwisho wa Gaddafi, Khamis, ambae ameripotiwa kuuwawa mara kadhaa tangu kuanza kwa mgogoro wa nchini humo, na haikuwahi kuthibitishwa, anaweza kuwa ameuwawa huko kusini mwa Tripoli na kuzikwa jana.
Khamis mwenye umri wa miaka 28, ametajwa kuwa kamanda madhubuiti katika majeshi ya Gaddafi.
Kiongozi wa waasi Mustafa Abdel Jalil amevitaka vikosi vya NATO kuongeza mbinyo zaidi dhidi ya Gaddafi akisema bwana huyo, bado kitisho, sio kwa Libya bali kwa dunia nzima.
Ikulu ya Marekani imesema haifahamu mahali alipo kiongozi huyo, ingawa ikaongeza kuwa hakuna viashiria vyoyote vinavyoonesha kama ameondoka nchini humo.
Kumekuwepo na hisia kwamba anaweza kuwepo katika kijiji alichozaliwa cha Sirte kilichopo kilometa 360 kutoka Tripoli ambapo pia wapiganaji waasi wanakijongelea kwa hivi sasa.
Wakati hayo yakiendelea baraza la waasi, leo hii litatarajiwa kuiwakisha Libya katika mkutano wa kimataifa utakaofanyika Paris, nchini Ufaransa. Kiongozi wa NTC Mustafe Abdel Jalil na ujumbe wake wa watu 40 wataudhuria mkutano huo
No comments:
Post a Comment