Monday, 1 August 2011

HALI YA MALAWI BADO SI SHWARI



 

Hali bado si shwari nchini Malawi, maduka yamefungwa, vikosi vya usalama vya vimetanda mitaani vikifanya doria na hasa katika miji mikubwa baada maandamano ya yaliyosabaisha vifo vya watu 18.

 
Marekani na Uingereza zimelaani ukandamizwaji unaofanywa na serikali dhidi ya waandamanaji pamoja na kitendo chake cha kuzidhibiti radio binafsi zinazojaribu kutangaza hali ya vurugu nchini humo.
Ubalozi wa Marekani nchini Afrika Kusini umesema kutokana na vurugu zinazoendelea na minong'ono ya vitendo vya  kulipiziana visasi, wamezitaka pande zote kuvumiliana.
Vurugu kama hizo ni kama hazijawahi kusikika nchini Malawi, ambayo imetawaliwa kwa miongo kadhaa na diktekta Kamuzu Banda baada ya kujipatia uhuru wake 1964.
Malawi sasa inaonekana kuingia katika mkumbo wa nchi za Afrika ya Kaskazini pamoja na Mashariki ya Kati ambazo katika kipindi cha miezi saba iliyopita hali imekuwa si shwari.
Simon Nzigamasabo ni mfanyabiashara ambae kwa hivi sasa yupo mjini Lilongwe, nchini Malawi, laakini yeye anasema maeneo hayo hali imeanza kurejea kuwa shwari.
Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Malawi, Henry Chimbali, amethibitisha kwamba vifo 10 vimetokea huko katika miji ya kaskazini ya nchi hiyo ya Kalonga na Mzuzu, ambapo waandamanaji waliokasirishwa na tatizo sugu la ukosefu wa mafuta na utawala wa Mutharika walizivamia na kufanya uharibifu katika ofisi za chama cha kiongozi huyo cha People Democratic Party( DPP) jumatano iliyopita.
Watu wengine wanane waliuwawa katika mji mkuu wa Lilongwe na Blantyre, baada ya polisi kujaribu kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya machozi. Waandamanaji hao pia walikuwa wakishinikiza Mutharika ajiuzulu kama kiongozi wa taifa hilo dogo lenye kiasi ya watu milioni 13.
Wachambuzi wanasema kuwa vurugu hizi za sasa zitamweka katika mahusiano mabaya zaidi na nchi wahisani na hasa Uingereza ambao ni wafadhili wakubwa, rais wa nchi hiyo, Bingu wa Mutharika, mchumi ambae ameingia madarakani 2004.
Hata hivyo, uwepo wa polisi na wanajeshi katika mitaa ya mji wa kibiashara wa Blantyre umepungua, magari yameanza kurudi barabarani na baadhi ya raia wanapanga kwenda katika mazishi ya waliouwawa katika maandamanao.
Mwandishi mmoja wa habari mjini Lilongwe, George Matonya amesema hali kwa asubuhi ya leo ilikuwa shwari, ingwa pia alionesha shaka kuhusu utulivu huo kwa wakati wa jioni

No comments:

Post a Comment