Tuesday, 30 August 2011
AMAIZING! HAVE U VISIT OUR NEW SOCIAL NETWORK?
NOW THERE IS NEW SOCIAL NETWORK SITE, NDONGOSINET IN THIS SITE YOU WILL BE ABLE TO FIND FRIENDS ACROSS THE WORLD, NOT ONLY THAT ALSO YOU WILL BE ABLE TO CHAT WITH THEM THROUGH WEBCAM, CALL, MESSAGE, ALSO TO SELL AND BUY PRODUCT ONLINE, WATCH MOVIES WITH DIFFERENT LANGUAGE INCLUDING SWAHILI LANGUAGE,UPLOAD, DOWNLOAD VIDEOS AND PICTURES, FORUM, AND MORE... THIS IS THE PROPER TIME FOR CHANGE WE HOPE YOU WILL ENJOY IT. YOU CAN ALSO VISIT OUR NETWORK BY CLICK THE LEFT HANDSIDE YOU WILL SEE GREEN WORDS WRITTEN NDONGOSINET CLICK THERE AND OUTOMATIC YOU WILL BE ON OUR SITE YOUR WELCOME
Waasi wataka kurejeshwa kwa mke wa Gaddafi kutoka Algeria
Akizungumza baada ya Algeria kutangaza kuwa mkewe Gaddafi, Safiya pamoja na watoto wawili wa kiume, binti yake na watoto wao wamevuka mpaka na kuingia nchni humo, Msemaji wa waasi, Mahmud Shammam alisema kwamba wangenda watu wote hao warejeshwe.
Mpaka sasa, Algeria haijalitambua baraza la waasi na imekuwa na msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mgogoro wa Libya, hata hivyo miongoni mwa waasi wamekuwa wakihituhumu nchi hiyo kuunga mkono utawala wa Gaddafi.
Katika taarifa iliyotangazwa na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, imetaja majina ya watoto wa Gaddafi ambao wamevuka mpaka Libya na kuingia Algeria kuwa ni Aisha, Hanibar na Mohammed.
Gaddafi akiwa na familia yakeHata hivyo haikutoa ufafanuzi zaidi kuhusu alipo Gaddafi mwenyewe. Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kwamba viongozi mbalimbali tayari wamekwisha fahamishwa kuhusu jambo hilo.
Miongoni wa waliotajwakupata taarifa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Baraza la Usalama la Umoja huo pamoja na Kiongozi namba mbili wa waasi wa Mahmud Jibril.
Akijibu taarifa hiyo, mbele ya waandishi wa habari mjini Tripoli Shammam amesema wanakipokea vyema kitendo hicho na kwamba wanawahakikishia majirani zao hao wanataka uhusiano mzuri baina yao kwa kuhakikisha wanawarejesha."Hicho ni kitendo cha uchokozi dhidi ya watu wa Libya na matumaini yao. Tutachukua njia zote za kisheria ili wahalifu hao warudishwa na baadae tutawapeleka mahakamani" alisema Shammam.
Nalo Shirika la Habari la ANSA, likinukuu vyanzo vya kuaminika vya kidiplomasia vya Libya vikisema Gaddafi Gaddafi na wanawe Saadi pamoja na Seif al-Islam wamejificha katika mji unaoitwa Bani Walid, uliyopo kusini mwa Tripoli.
Katika hatua nyingine Waziri wa Sheria katika Baraza la Waasi, Mohammed al-Allagy amesema mtoto wa mwisho wa Gaddafi, Khamis, ambae ameripotiwa kuuwawa mara kadhaa tangu kuanza kwa mgogoro wa nchini humo, na haikuwahi kuthibitishwa, anaweza kuwa ameuwawa huko kusini mwa Tripoli na kuzikwa jana.
Khamis mwenye umri wa miaka 28, ametajwa kuwa kamanda madhubuiti katika majeshi ya Gaddafi.
Kiongozi wa waasi Mustafa Abdel Jalil amevitaka vikosi vya NATO kuongeza mbinyo zaidi dhidi ya Gaddafi akisema bwana huyo, bado kitisho, sio kwa Libya bali kwa dunia nzima.
Ikulu ya Marekani imesema haifahamu mahali alipo kiongozi huyo, ingawa ikaongeza kuwa hakuna viashiria vyoyote vinavyoonesha kama ameondoka nchini humo.
Kumekuwepo na hisia kwamba anaweza kuwepo katika kijiji alichozaliwa cha Sirte kilichopo kilometa 360 kutoka Tripoli ambapo pia wapiganaji waasi wanakijongelea kwa hivi sasa.
Wakati hayo yakiendelea baraza la waasi, leo hii litatarajiwa kuiwakisha Libya katika mkutano wa kimataifa utakaofanyika Paris, nchini Ufaransa. Kiongozi wa NTC Mustafe Abdel Jalil na ujumbe wake wa watu 40 wataudhuria mkutano huo
Majeshi ya Gaddafi yatakiwa kusalimu amri
Viongozi wa waasi wa Libya wamewapa majeshi yanayomwuunga mkono Kanali Gaddafi mpaka Jumamosi kusalimu amri au kukabiliana na majeshi.
Mustafa Abdul Jalil, anayeongoza Baraza la Mpito la Taifa (NTC), alisema onyo hilo limeelekezwa kwa wanaomtii Kanali Muammar Gaddafi waliopo mji alipozaliwa wa Sirte na katika miji mengine.
Tangazo hilo limetolewa baada ya mke wa Kanali Gaddafi na watoto wake watatu kukimbilia nchi jirani ya Algeria.
Algeria imejitetea kwa hatua hiyo waliochukua, huku waasi wakiita " kitendo cha kiburi".
Mpaka sasa mahala alipo Kanali Gaddafi haijulikani.
Wakati huo huo huo huko Libya, waasi wanajaribu kupambana na wanaomtii Gaddafi, na kujiandaa kusogea Sirte.
CCM WACHUANA NA CHADEMA KWA KUTUMIA CHOPPER
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemtangaza Dk Dalaly Kafumu kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo wa Igunga huku pia kikitangaza kutumia helikopta kupiga kampeni za anga kwa anga ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha jimbo hilo haliangukii kwenye himaya ya upinzani.
Hatua ya CCM kutangaza kutumia helikopta inakuja wakati tayari Chadema, nacho tayari kikiwa kimetangaza kutumia usafiri huo wa anga kufika maeneo mengi katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2 kuziba nafasi ya Rostam Aziz, aliyejiuzulu wadhifa huo mnamo mwezi Julai.
Wakati vyama vingine vya upinzani vikiwa vimemaliza mchakato wa kupata wagombea wao, jana CC ya CCM ilikutana jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, ambayo pamoja na mambo mengine ilimtangaza Dk Kafumu ikiwa ni kukamilisha mchakato huo ulioanzia ngazi ya wilaya.
Utaratibu wa CCM, mgombea ubunge huanza kupigiwa kura na wajumbe wa kuanzia wilaya kisha mkoa na kutoa alama pasipo kukata jina hata moja na mwisho CC chini ya mwenyekiti, hufanya maamuzi ya mwisho.
Hadi sasa tayari CUF wamempitisha Leonard Mahona, ambaye alichuana na Rostam mwaka jana na kupata kura 11,000, Chadema ni Joseph Kashindye, Moses Edward (TLP) na John Maguma wa Sau, huku uchukuaji fomu ukiwa tayari umeanza tangu Agosti 24 na kutarajiwa kukamilika Septemba sita.
Vyama vya upinzani vikikamilisha mchakato na uchukuaji fomu ukiwa umeanza, jana Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM, Nape Nnauye, ilitangaza uamuzi huo wa CC wa kumpitiisha Dk Kafumu, ambaye tayari aliwahi kugombea na Rostam mara mbili katika kura za maoni ndani ya chama bila mafanikio.
Nape alitamba kwamba CCM inaingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na matumaini makubwa ya kushinda huku kauli mbiu ikiwa ni, "Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele.”
Mkapa kuzindua kampe
Alifafanua kwamba mbali ya uamuzi wa kumpitisha Dk Kafumu, kikao hicho cha CC kilimpitisha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa kuzindua kampeni za chama hicho, zitakazoanza mwezi ujao.
“Kampeni hizo zitazinduliwa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamini Mkapa wakati muafaka wa kampeni utakapowadia,” alisema Nape na kuongeza tambo akisema CCM itashinda uchaguzi huo kwa kishindo.
Sababu za kushinda wanazo
Alitaja sababu nne ambazo alizielezea ni miongoni mwa nyingi zinazokipa chama hicho tawala jeuri ya ushindi kwenye uchaguzi huo, ambazo ni pamoja na tathmini waliyoifanya katika siku za karibuni na kubaini wanachama wake katika jimbo hilo wana mshikamano mkubwa na mapenzi kwa chama chao.
Nape aliitaja sababu nyingine ni kwamba, katika uchaguzi wa kura za maoni walizofanya siku za karibuni jimboni humo zilionekana kuwa na utulivu na hakukuwepo na makundi yenye msuguano kama ilivyokwishawahi kutokea kwenye baadhi ya majimbo ambayo CCM iliyapoteza kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Katika kudhihirisha hilo, Nape alisema hata wagombea walioshindwa kwenye kura za maoni walikuwa jijini Dar es Salaam na waliahidi kuwa watashirikiana na Dk Kafumu katika kufanikisha ushindi wa CCM.
“Katika kufanikisha kampeni za CCM, wanachama waliowania kuteuliwa katika nafasi hiyo wameahidi watashiriki kikamilifu katika kampeni hizo,” akisema hiyo ni ishara ya mshikamano wa wana CCM Igunga.
Wagombea wanaotarajia kumuunga mkono DK Kafumu ambaye aliibuka mshindi wa kura za maoni, 588, ni aliyemfuatia kwa karibu Jafari Omari aliyepata 193 na Shams Brahamu, aliyepata kura 38 kati ya wagombea jumla 13 walioshiriki uchaguzi huo kuomba ridhaa ya chama hicho tawala na kikongwe barani Afrika.
Nape akisisitiza sababu za ushindi katika uchauguzi huo, alisema ni pamoja na CCM kuwa na mizizi imara iliyojikita katika vitongoji vyote vya jimbo hilo, tofauti na vyama vya upinzani.
“CCM ipo Igunga wakati wote (wa uchaguzi na usio wa uchaguzi). Vyama vya upinzani huonekana kule tu wakati wa uchaguzi,” alisema Nape na kuongeza kwamba hiyo ndiyo sababu inayovifanya vyama hivyo vya upinzani kutumia nguvu nyingi wakati wa uchaguzi.
CCM Wilaya, mkoa kuongoza mashambulizi
Alisema tofauti na vyama vya upinzani, katika uchaguzi wa Igunga, CCM Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Igunga ndio watakaosimamia kampeni za chama hicho.
Nape alisema hali hiyo ni tofauti na vyama hivyo vya upinzani ambavyo huhamishia viongozi wake wote wa kitaifa kwenye chaguzi ndogo ili kujenga nguvu.
“Vyama vya upinzani wao huhamishia viongozi wake wote wa makao makuu hadi walinzi wa ofisi ili kupiga kampeni,” alidai.
Aliongeza, “Sisi hatuna haja hiyo. Kama akiwepo kiongozi wa juu, anakuwa anapita tu. Haendi kuweka kambi.”
Alisema kiongozi wa ngazi za juu kabisa anayeweza kuwepo kwenye kampeni za CCM Igunga kwa muda wote ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye ni mlezi wa chama hicho Wilaya ya Igunga.
Hata hivyo, ingawa Nape ametoa sababu hizo za kuachia uongozi wa wilaya na mkoa, lakini moja ya mambo yaliyojadiliwa kwenye CC iliyoketi mjini Dodoma mwezi uliopita ilimpiga marufuku katibu huyo na baadhi ya makada wake wenye mlengo kama wake kutoshiriki kampeni hizo kutokana na hali halisi ya siasa za makundi ndani ya chama hicho.
Uamuzi huo wa CC ulilenga kuepusha uwezekano wa CCM kulipoteza jimbo hilo endapo baadhi ya watu waliokuwa wakimshambulia Rostam kama wangeshirikishwa kwenye kampeni za uchaguzi huo na kuondoa umoja na mshikamano.
CCM kutumia helikopta
Kwa mujibu wa Nape, CCM itaingia katika uchaguzi kwa kutumia helikopta kutokana na jiographia ya jimbo hilo.
“Tunaenda kuwaeleza historia ya jimbo hilo, tumetoka wapi, tupo wapi na tunaenda wapi,” alisema Nape na kuongeza hilo litandamana na jinsi utekelezaji wa sera za CCM umefanyika kwenye jimbo hilo.
Wednesday, 17 August 2011
Monday, 15 August 2011
Tuesday, 9 August 2011
moja ya nyumba iliyochomwa moto katika fujo mjini london
Moto unaendelea kuwaka mjini London kwa siku ya tatu mfululizo wakati ghasia na hali isiyo tulivu vikiongezeka. Waziri mkuu David Cameron amekatisha mapumziko yake nchini Italia na kurejea mjini humo na anatarajiwa kukutana na kamati ya ngazi ya juu ya kushughulikia masuala ya dharura leo Jumanne. Wakati huo huo , ghasia hizo , ikiwa ni pamoja na uporaji ,uchomaji magari na majengo , umesambaa katika maeneo mapya mjini London na katika miji ya Birmingham na Liverpool. Ghasia hizo zilianzia Tottenham siku ya Jumamosi baada ya maandamano dhidi ya polisi kugeuka kuwa ghasia. Hata hivyo waziri wa mambo ya ndani Theresa May ameshutumu ghasia hizo kuwa ni uhalifu.Waziri mkuu David Cameron amekatiza mapumziko yake nchini Italia na kurejea mjini London.
Sunday, 7 August 2011
Monday, 1 August 2011
HALI YA MALAWI BADO SI SHWARI
Marekani na Uingereza zimelaani ukandamizwaji unaofanywa na serikali dhidi ya waandamanaji pamoja na kitendo chake cha kuzidhibiti radio binafsi zinazojaribu kutangaza hali ya vurugu nchini humo.
Ubalozi wa Marekani nchini Afrika Kusini umesema kutokana na vurugu zinazoendelea na minong'ono ya vitendo vya kulipiziana visasi, wamezitaka pande zote kuvumiliana.
Vurugu kama hizo ni kama hazijawahi kusikika nchini Malawi, ambayo imetawaliwa kwa miongo kadhaa na diktekta Kamuzu Banda baada ya kujipatia uhuru wake 1964.
Malawi sasa inaonekana kuingia katika mkumbo wa nchi za Afrika ya Kaskazini pamoja na Mashariki ya Kati ambazo katika kipindi cha miezi saba iliyopita hali imekuwa si shwari.
Simon Nzigamasabo ni mfanyabiashara ambae kwa hivi sasa yupo mjini Lilongwe, nchini Malawi, laakini yeye anasema maeneo hayo hali imeanza kurejea kuwa shwari.
Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Malawi, Henry Chimbali, amethibitisha kwamba vifo 10 vimetokea huko katika miji ya kaskazini ya nchi hiyo ya Kalonga na Mzuzu, ambapo waandamanaji waliokasirishwa na tatizo sugu la ukosefu wa mafuta na utawala wa Mutharika walizivamia na kufanya uharibifu katika ofisi za chama cha kiongozi huyo cha People Democratic Party( DPP) jumatano iliyopita.
Watu wengine wanane waliuwawa katika mji mkuu wa Lilongwe na Blantyre, baada ya polisi kujaribu kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya machozi. Waandamanaji hao pia walikuwa wakishinikiza Mutharika ajiuzulu kama kiongozi wa taifa hilo dogo lenye kiasi ya watu milioni 13.
Wachambuzi wanasema kuwa vurugu hizi za sasa zitamweka katika mahusiano mabaya zaidi na nchi wahisani na hasa Uingereza ambao ni wafadhili wakubwa, rais wa nchi hiyo, Bingu wa Mutharika, mchumi ambae ameingia madarakani 2004.
Hata hivyo, uwepo wa polisi na wanajeshi katika mitaa ya mji wa kibiashara wa Blantyre umepungua, magari yameanza kurudi barabarani na baadhi ya raia wanapanga kwenda katika mazishi ya waliouwawa katika maandamanao.
Mwandishi mmoja wa habari mjini Lilongwe, George Matonya amesema hali kwa asubuhi ya leo ilikuwa shwari, ingwa pia alionesha shaka kuhusu utulivu huo kwa wakati wa jioni
Subscribe to:
Posts (Atom)